Sunday 17 February 2013

MAKE UP IDEAS


NATARAJIA KUTUA NCHINI MWEZI WA SITA MWAKA HUU NITAKUJA NA MZIGO MPYA WA MAVIPODOZI HASAHASA MAKE UP ZA UHAKIKA KUTOKA NCHINI INDIA. KWA RANGI YA MWEUSI,MWEUPE NA MAJI YA KUNDE.
PIA NINA TUBE ZA KUONDOA CHUNUSI KWA MUDA WA WIKI MBILI TU NI NATURAL HERBAL (AYURVEDIC).

karibuni mwembechai kituoni kabisa nitatoa namba yangu ya simu nikifika Tanzania ili iwe rahisi kuwasiliana kwa wale wahitaji.

NAMNA YA KUONDOA CHUNUSI SUGU USONI


Chunusi husababishwa na kuongezeka kwa uzalishaji wa Testosterone hormone na mafuta yamwili wakati wa mabadiliko ya kimwili pia husababishwa na msongo wa mawazo, matatizo ya kisaikolojia.

Product kama Tea Tree Oil, Aloe Vera, Zinc, and Vitamin A ni vitu vya kihalisi vinavyo weza kutibu chunusi na kuna baadhi ya product hazishauriwi kutumiwa na mtu kama unaujauzito au unatatizo la kiafya hivyo unatakiwa kuwasiliana na dactari kabla ya kutumia kwa ushauri.
Kabla ya kuoga ponda nyanya changanya na asali na maji ya roses na paka nyanya kwenye uso wako kaa nayo kwa muda wa dakika 20 kabla ya kuosha.
Usiku kabla ya kulala paka mchanganyiko wa cream, glycerine, and lemon juice kwenye uso wako na kaa nayo kwa muda wa dakika chake kabla ya kuosha.
Pia jambo la muhumu kwa mtu anayesumbuliwa na chunusi ni kunywa maji kwa angalau lita 3 kila siku pia ni muhimu sana kwa ngozi yako, matunda fresh na mboga za majani kwenye diet yako.
Vitu unavyotakiwa kuepuka ni kugusa uso wako mara kwa mara, epusha nywele kugusa uso wako na kutumbua chunusi kiholela.

 NJIA KUMI ZA KUWA MJASILIAMALI


1. MAWASILIANO NA WAJASIRIAMALI WENGINE
Jenga urafiki nao kuwa karibu nao mara kwa mara maana mnafanana katika biashara, toka nao kwenda sehemu mbali mbali ili uweze kujifunza mengi kutoka kwao.
2. DAIMA JIAMINI
Amini kuwa kile unachokifanya kipo sahihi na sio kama una bahatisha
3. MATANGAZO NA SOKO
Tangaza biashara yako ili uweze kupata wateja wengi zaidi na kuweza kujulikana haraka, soko linakuja kama utakuwa unafahamika.
4. KUTAFUTA NJIA RAHISI
Usitumie pesa nyingi sana maana biashara yako ndio kwanza inaanza kwa hiyo unahitajika kuangalia njia rahisi ya kuweza kubana matumizi yako.
5. KUUNGANA NA WAJASIRIAMALI WENGINE KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII
Kuna mitandao mingi ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, My Space n.k ni vema kuitumia hii kama kiunganishi kikubwa na wajasiriamali wengine na wateja ili kuweza kuongeza maendeleo.
 
 6. KUTENGENEZA WEBSITE YAKO
Kuwa na site yako binafsi ni nzuri maana itasaidia kufanya kazi kwa urahisi na kisasa kabisa, fungua website yako na uweke bidhaa zako ili uweze kuwavutia wateja wako.
7. KUJIFUNZA MAKOSA
Angalia pale ulipokosa na ujifunze usije kurudia tena lile kosa la mwanzo.
8. KUFANYA KIPAJI CHAKO KAMA KAZI YAKO
Chukulia unachokifanya ni kama kazi yako yani kama vile waziri anavyotoka kwake na kwenda Wizarani kazini.
9. KUHUDHURIA SEMINA
Kuhudhuria semina mbali mbali za mafunzo ya ujasiriamali ili kupata knowledge zaidi.
10. TAFUTA MBINU RAHISI YA KUTATUA TATIZO KUBWA
Siku zote ona tatizo kubwa kama la kawaida sana na usipanic ona ni jambo rahisi sana usijijengee kushindwa.